Historia Yetu
“Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.” — Waefeso 3:20–21
Kanisa lilianzishwa mnamo mwaka 2019 mkoani Mwanza, Tanzania, chini ya Mchungaji Samwel Hamisi pamoja na mke wake Sarah Samwel, kama kusanyiko dogo lililokuwa likifanya ibada zake kwenye nyumba ya mmojawapo wa washirika. Huduma ilisimama kwa muda baada ya mchungaji kuhamia sehemu nyingine iliyoitwa Mahina Nyangulugu.
Mungu aliendelea kuweka msukumo wa huduma ndani ya moyo wa Mchungaji Samwel, ndipo alipoamua kuendelea na huduma kwa kufanya ibada ya kwanza tarehe 17 Mei 2020 katika nyumba aliyokuwa amepanga, akiwa na washirika watatu: mke, mtoto na shemeji yake.
Baada ya hapo huduma ikahamia kwenye jengo la shule ambapo, ndani ya muda mfupi, kupitia uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, washirika waliongezeka hadi kufikia watu hamsini, hali iliyolazimu kuhamia kwenye eneo jingine.
Ashukuriwe Mungu, hadi sasa kanisa lina jumla ya washirika 400, wakubwa na watoto. Kutokana na kupanua maono ili kuwafikia watu wengi zaidi Tanzania na nje ya mipaka yake, ikalazimu kubadili jina kutoka Hossana Gospel Church (HGC) na kuitwa Hossana International Community Church (HICC).
Safari yetu
-
2019
Mwanzo Kusanyiko dogo nyumbani kwa mshirika, Mwanza.
-
2019–20
Kuhamia Mahina Huduma inasimama kwa muda mchungaji anapohamia Mahina Nyangulugu.
-
17 Mei 2020
Ibada ya kwanza Washirika watatu katika nyumba ya kupanga.
-
2020+
Jengo la shule Uinjilisti wa nyumba kwa nyumba; washirika 50.
-
—
HGC inakuwa HICC Jina jipya kwa maono ya kimataifa.
-
2026
Washirika 400 Wakubwa na watoto, na maono ya matawi.