Historia Yetu
Kutoka watu wanne kwenye nyumba ya kupanga hadi familia ya washirika 400.
Kanisa lilianzishwa mnamo mwaka 2019 mkoani Mwanza, Tanzania, chini ya Mchungaji Samwel Hamisi pamoja na mke wake Sarah Samwel, kama kusanyiko dogo lililokuwa likifanya ibada zake kwenye nyumba ya mmojawapo wa washirika. Huduma ilisimama kwa muda baada ya mchungaji kuhamia sehemu nyingine iliyoitwa Mahina Nyangulugu.
Mungu aliendelea kuweka msukumo wa huduma ndani ya moyo wa Mchungaji Samwel, ndipo alipoamua kuendelea na huduma kwa kufanya ibada ya kwanza tarehe 17 Mei 2020 katika nyumba aliyokuwa amepanga, akiwa na washirika watatu: mke, mtoto na shemeji yake.
Baada ya hapo huduma ikahamia kwenye jengo la shule ambapo, ndani ya muda mfupi, kupitia uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, washirika waliongezeka hadi kufikia watu hamsini, hali iliyolazimu kuhamia kwenye eneo jingine.
Ashukuriwe Mungu, hadi sasa kanisa lina jumla ya washirika 400, wakubwa na watoto. Kutokana na kupanua maono ili kuwafikia watu wengi zaidi Tanzania na nje ya mipaka yake, ikalazimu kubadili jina kutoka Hossana Gospel Church (HGC) na kuitwa Hossana International Community Church (HICC).
Tulikotoka
-
2019
Mwanzo
Kusanyiko dogo linaanza kuabudu nyumbani kwa mshirika mmoja, Mwanza.
-
2020
Ibada ya kwanza
17 Mei 2020: ibada ya kwanza katika nyumba ya kupanga, watu wanne.
-
Baadaye
Jengo la shule
Kupitia uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, washirika wanafikia 50.
-
Leo
HICC
Washirika 400. Jina linabadilika kutoka Hossana Gospel Church kuwa Hossana International Community Church.